Home » » BAJETI YA NISHATI YAPITA KWA MBINDE.

BAJETI YA NISHATI YAPITA KWA MBINDE.

Mbunge wa Simanjiro Chrisptopher Ole- Sendeka, akionyesha ripoti ya Mkaguzi Ernest&Young kuhusu Shirika la Umeme nchini na kudanganywa kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kulik
ofanywa na watendaji wake, wakati wa uchangiaji wa mjadala wa Nishati na Madini, bungeni Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman.

 
BAJETI ya Wizara ya Nishati na Madini imepita kwa mbinde, huku Bunge likiunda kamati maalumu kuchunguza chanzo cha mgororo wa gesi mkoani Mtwara.
Bajeti hiyo imepita baada ya Waziri Profesa Sospeter Muhongo kufanikiwa kuzima kusudio la wabunge saba waliotaka kuikwamisha kwa kuondoa shilingi kama hoja zao hazijapata majibu ya kuridhisha.
Wabunge waliotishia kuondoa shilingi kwenye bajeti hiyo ni John Mnyika (Ubungo), Ezekiah Maige (Msalala), Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Nimrodi Mkono (Musoma Vijijini) James Lembeli (Kahama), Dk Khamis Kigwangalla (Nzega) na Tundu Lissu (Singida Mashariki).
Wabunge hao walitaka kuikwamisha bajeti hiyo kutokana na hoja mbalimbali,huku wengi wao wakitaka majibu ya miradi ya utekelezaji wa mradi wa Rea kwenye majimbo hayo.
Waziri Muhongo akisaidiana na manaibu wake, George Simbachawene na Steven Masele walifanikiwa kupangua hoja za wabunge hao kwa kueleza mipango ya wizara katika kutekeleza madai yao na kuifanya bajeti hiyo ikose upinzani.
www.mwananchi.co.tz

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa