Home » » IBADA MAALUMU YA BUNGE LA KATIBA LEO DOM

IBADA MAALUMU YA BUNGE LA KATIBA LEO DOM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Wakati viongozi wa dini wakipaza sauti kutaka maoni ya wananchi kuheshimiwa, Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma, leo litaendesha sala maalumu ya kuliombea Bunge Maalumu la Katiba.
Ibada hiyo ambayo itafanyika saa 7 mchana katika kanisa lililopo ndani ya maeneo ya Bunge, itaendeshwa na Askofu wa Jimbo la Dodoma, Mhashamu Askofu Gervas Nyaisonga.
Kuendeshwa kwa ibada hiyo maalumu, kulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samiah Suluhu Hassan.
“Atakuja kusali katika kanisa la hapa bungeni saa 7 mchana kwa lengo la kuliombea Bunge Maalumu…Wakristo wote tunaombwa kujumuika katika sala hii,” alisema.
Ibada hiyo inaendeshwa zikiwa zimepita siku chache tu baada ya Maaskofu 32 wa kanisa hilo kutoa waraka maalumu wa Pasaka kwa wajumbe wa Bunge hilo wakiwataka kuheshimu maoni ya wananchi.
Maaskofu hao walisema ili kupata Katiba bora, wajumbe wanapaswa kuheshimu kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuitumia kama ilivyokusudiwa na sheria.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa