Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MCHUNGAJI wa Kanisa la PAG, Charles Kanyika, amemtaka Rais Jakaya
Kikwete, kushirikiana na viongozi wastaafu kunusuru nchi katika kipindi
hiki cha kuelekea kutunga Katiba mpya.
Mchungaji Kanyika alisema Rais Kikwete alianza kuiweka nchi katika
hatua mbaya baada ya kutoa hotuba ya kufungua Bunge Maalumu, iliyokuwa
na lengo la kutetea msimamo wa chama anachotoka.
“Tunakoelekea hawa viongozi wa siasa watatuingiza mahali pabaya
wamekuwa wakitoa matamko ambayo yanawachanganya wananchi na kuhusu huu
mchakato kuna kila sababu akawahusisha viongozi ambao ni maarufu ili
wakae meza moja ili kutafuta mwafaka.
“Jambo la msingi na la muhimu ni kuwaomba marais wastaafu pande zote
mbili mawaziri wakuu pande zote mbili na majaji na wanasheria pande
zote mbili kukaa meza moja na ili kufanikiwa mwenyekiti wa kikao hicho
awe rais wa Pili Ali Hassan Mwinyi,” alitoa ushauri huo Mchungaji
Kanyika.
Alisema anawapongeza wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA) kwa kususia mijadala ya Bunge kwa kuwa kilichokuwa kikijadiliwa
ni msimamo wa CCM badala ya rasimu iliyowasilishwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba.
“Kinachotakiwa kujadiliwa si serikali mbili, wajumbe wanatakiwa
kujadili kile kilichopo katika rasimu ya Katiba ambayo ni serikali
tatu, hayo si mawazo ya tume bali ni mawazo ya wananchi,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment