Home » » MAMA SALMA AZINDUA RASMI UCHUNGUZI WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI WILAYA YA BAHI - MKOANI DODOMA.

MAMA SALMA AZINDUA RASMI UCHUNGUZI WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI WILAYA YA BAHI - MKOANI DODOMA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Ndugu Betty Mkwasa mara baada ya kuwasili mjini Bahi kushiriki mkwenye sherehe ya uzinduzi wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi na wananchi wa Bahi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa saratani ya shingo ya kizazi mjini hapo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa Macho wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Frank Magupa, wakati alipotembelea maonesho ya kitabibu yaliyofanyika sambamba na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa wilayani Bahi.
 Mamia ya wananchi wa Bahi wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na viongozi wa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi iliyofanyika huko Bahi, Mkoani Dodoma
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Kebwe Staphen Kebwe akitoa salamu hotuba kwa niaba ya wizara ya Afya wakati wa uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi huko wilayani Bahi.
 Mamia ya wananchi wa Bahi wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na viongozi wa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi iliyofanyika huko Bahi, Mkoani Dodoma.
 ke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Bahi muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi kampeni ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
 ke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa Wilaya ya Bahi.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha vifaa mbalimbali vinavyotumika na madaktari wakati wa kuwapima wanawake ili kufahamu kama wana maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo wilayani Bahi.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wacheza ngoma na wananchi mbalimbali wa wilaya ya Bahi mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa akinamama.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Bwana Hamis Mwege kwa kazi kubwa ya kuelimisha umma kuhusu kampeni ya kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake hapa nchini. Vyombo vingine vilivyopata cheti ni Channel Ten na ITV.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Bahi mara baaada ya kuzindua rasmi mapambano ya kutokomeza maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake. 
PICHA NA JOHN  LUKUWI

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa