Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema vyanzo vya
mapato vilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba, havitoshi kuendesha
Serikali ya shirikisho.
Nchemba aliyasema hayo katika kipindi cha Tuongee, kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star TV kila asubuhi.
“Sijui kama ilikuwa ni makusudi Serikali ya
shirikisho itengenezwe halafu iishie njiani, kwanza tafsiri ya ushuru wa
bidhaa ni finyu,” alisema. Kwa mujibu wa Mwigulu tafsiri ya ushuru wa
bidhaa inajumuisha forodha, ushuru wa bidhaa, kodi ya mauzo, kodi ya
ongezeko la thamani (VAT), kodi ya mazao na kodi ya mauzo ya nje.
Alisema kwa tafsiri hiyo pana, makadirio yake yanaweza kwenda hadi Sh4 trilioni na kuendelea.
Hata hivyo, aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, Humphery Polepole alisema waliziita taasisi zote za fedha na
kupata nafasi ya kujua makusanyo, matumizi na jinsi matumizi ya
muungano yanavyokuwa.
Polepole alisema kulingana na uchambuzi
walioufanya, fedha inayotakiwa kuendesha Serikali ya shirikisho ipo na
kwamba mapato hayo yanatosha kuendesha Serikali hiyo.
Alisema imethibitika matumizi makubwa ya fedha
yanatumika Tanzania Bara kuliko Zanzibar na gharama za Muungano ambazo
ni Sh1.8 trilioni ni ndogo ikilinganishwa na zile za pande zote mbili za
Muungano.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment