Home » » PENGO LA MASKINI,TAJIRI KACHAFUA NCHI

PENGO LA MASKINI,TAJIRI KACHAFUA NCHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MKUU wa Wilaya ya Kongwa, Alfred Msovela, amesema kuna uwezekano wa taifa kuingia katika machafuko kutokana na kuwepo kwa matabaka ya wenye nacho na wasiokuwa nacho.
Alisema kutokana na wachache kuwa na maisha mazuri huku wengi kuwa na maisha mabaya ndiko kumesababisha baadhi ya watu kuona bora kuishi mijini na wengine vijiji.
Msovella alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa mradi wa TASAF awamu ya tatu uliodhamiria kupambana na kaya maskini zaidi nchini zikiwemo zile za Wilaya ya Kongwa.
Alisema kuna kauli mbalimbali zinazomtambulisha mtu anayeishi kijijini kama mkulima na kudai kuwa kilimo ni uti wa mgongo na kauli mbalimbali bila kujali kuwa mkulima huyo anatumia nyenzo gani katika kuendeleza shughuli zake.
“Wapo viongozi ambao wanadhani kuwa na wakulima wengi ndiyo kuwa na wakulima wenye maisha bora na wazalishaji wa chakula cha kutosha, kimsingi wakulima wanaweza kuwa wengi lakini wakaendelea kuwa maskini kutokana na kutoweza kulima kisasa, wanalima kujikimu,” alisema Msovella.
Akizungumzia kuhusu misaada ambayo inatolewa na TASAFIII kwa familia maskini alisema atapambana na watumishi ambao wataonekana kufanya udanganyifu kwa kushindwa kuwafikia walengwa.
Kwa upande wa uongozi wa TASAF, wamesema kuwa katika mradi huo wanakusudia kuwaondolea umaskini watu milioni 7.5 nchi nzima sawa na kaya milioni 1.2.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa