Home » » TASAF III KUZIFIKIA KAYA MILIONI 1.2

TASAF III KUZIFIKIA KAYA MILIONI 1.2

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
KAYA milioni 1.2 zinatarajiwa kufikiwa na mpango wa serikali wa kusaidia kaya masikini awamu ya tatu (TASAF III) ili kuzinusuru katika Wilaya ya Chamwino, Dodoma.
Akizungumza kwenye warsha ya kutoa uelewa kwa madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAF, Zuhura Mdungi, alisema mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka 10 katika awamu mbili za miaka mitano mitano.
“Utekelezaji wa mpango huo unahitaji uwekezaji mkubwa kwenye mifumo na kujenga uwezo katika ngazi zote. Utatekelezwa kwenye maeneo machache na kuongeza kadiri ya uwezo unavyojengeka,” alisema Zuhura.
Akielezea kuhusu madhumuni ya mpango huo, alisema ni kuwezesha kaya masikini sana kuongeza matumizi muhimu kwa njia endelevu, kuziwezesha kwa matumuzi ya lazima ya binadamu na kuwekeza kwenye rasilimali watu, hususan kusomesha watoto.
Madhumuni mengine ni kuimarisha shughuli za kuongeza kipato na matumizi ya huduma za jamii huku akibainisha kwamba Rais Jakaya Kikwete alizundua mpango huo Februari 2013 mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo, mpango wa kunusuru kaya masikini umeganyika katika maeneo mbalimbali ambayo ni kutoa ruzuku kwa kaya masikini sana, hususan zenye wajawazito na watoto ili zipate elimu na afya, lakini pia kutoa ajira kwa kaya zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi wakati wa majanga mbalimbali.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa