Home » » UKAWA:ALAT YA VURUGA RASIMU YA KATIBA

UKAWA:ALAT YA VURUGA RASIMU YA KATIBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwenykiti wa Ukawa,Freeman Mbowe.
 
Shirikisho la Serikali za Mitaa (Alat) limetuhumiwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuvuruga Rasimu ya Katiba kwa kuleta mawazo mapya.
Uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba umeikana semina hiyo kuwa haiifahamu na siyo halali.

Alat inalaumiwa kutoa semina kwa wajumbe wa Bunge Maalumu, kinyume cha sheria na utaratibu na kuwashawishi kuingiza vipengele vya umuhimu wa serikali za mitaa kwenye rasimu ya katiba.

Mwenykiti wa Ukawa, Freeman Mbowe, pamoja na viongozi wengine, James Mbatia, na Tundu Lissu, walisema jana mjini hapa, wakati shirikisho hilo likiendelea kutoa semina kwa wajumbe.

Mbowe alisema ni kinyume cha sheria kuchakachua rasimu, ambayo kwa mujibu wa sheria ya marekebisho ya katiba namba 83 ya 2013 hairuhusiwi kuingiza jambo jipya nje ya utaratibu.

Walionya kuwa Alat kuleta vifungu vingine na kuviingiza kwenye rasimu  kupitia semina ni ukiukaji wa sheria.

“Alat ilitakiwa kutoa mapendekezo kwenye Tume ya Marekebisho ya Katiba si kutoa semina na kuleta mapendekezo mapya kinyemela,” alionya Mbowe.

Aliongeza: “Tunaitaka Alat isikiuke taratibu za kisheria pia CCM na serikali isitumie hila kulazimisha ajenda za serikali mbili kupitia semina hizi.”
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa