Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Hawra Shamte
Wasemaji wamesema, wadadavuaji wamedadavua, wapangaji wamepanga
na bado jambo hili limeendelea kuwa hadithi. Serikali ya Tanzania
iliamua kubadilisha makao makuu yake tangu mwaka 1976, sasa ni miaka 38,
uamuzi huo bado haujatekelezwa.
Kuna wakati Serikali ilijikakamua, ikajenga
majengo ya wizara kadhaa mjini Dodoma kwa dhamira ya kuhamishia utendaji
wa wizara hizo makao makuu pendekezwa, baadhi ya wizara zilihamia
Dodoma, lakini taratibu wizWasemaji wamesema, wadadavuaji wamedadavua,
wapangaji wamepanga na bado jambo hili limeendelea kuwa hadithi.
Serikali ya Tanzania iliamua kubadilisha makao makuu yake tangu mwaka
1976, sasa ni miaka 38, uamuzi huo bado haujatekelezwa.ara hizo
zikajikuta zinarudisha majukumu yake yote makubwa Dar es Salaam.
Serikali ikidhamiria kiukweli, Dar es Salaam
inaweza kubaki kuwa Jiji la biashara na Dodoma ukawa ni mji mkuu wa
shughuli za Serikali. Serikali ikitaka kufanya hivyo, isiwahamishe
watumishi tu wa wizara zake, bali inapaswa kwanza imhamishe Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyo akihamia Dodoma kila wizara
itahamia tena kwa nguvu zote.
Wiki iliyopita, mbunge wa Chilonwa (CCM), Hezekiah
Chibulunje aliulizia tena dhamira ya Serikali kuhamia Dodoma, yeye
alishangazwa na kitendo cha Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Ushirika
ambayo ina majengo yake Dodoma, hivi sasa shughuli zake nyingi
zimesharudishwa Dar es Salaam. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Sophia
Simba alijibu swali la Chibulunje kisiasa, kama ambavyo miaka yote
linavyojibiwa kisiasa kwamba dhamira ya Serikali bado iko palepale.
Mbunge mwingine alitoa pendekezo kuhusu nyumba za
watumishi wa Ikulu ambazo kwa muda mrefu zinakuwa tupu kwa maana ya kuwa
hakuna watumishi wanaozitumia, hoja ilikuwa nyumba hizo ziwe chini ya
mamlaka ya halmashauri ya wilaya ya Chamwino ili watumishi wake wapate
makazi.
Jibu lililotolewa ni kuwa nyumba hizo ni za
watumishi wa Ofisi ya Rais ambao wanakuwapo Dodoma rais akienda Dodoma,
hivyo haziwezi kugawiwa kwa taasisi nyingine yoyote ile.
Tunaweza kuangalia safari za Rais Dodoma ni mara ngapi kwa mwaka na huwa anakaa kwa siku ngapi?
Ikiwa idadi ya safari zake ni kidogo na siku
anazokuwapo Dodoma ni chache, binafsi sioni haja ya kuwapo kwa nyumba
maalumu kwa ajili ya watumishi wa Ofisi ya Rais. Kama haja hiyo ipo,
basi ni bora zaidi ikiwa Rais atakuwa anaishi Dodoma.
Rais akihamia Dodoma, ofisi zote za Serikali
zitahamia huko, ofisi zote za ubalozi zitahamia huko kwa sababu huko
ndiko kwenye kitovu cha nchi na Dar es Salaam litakuwa ni jiji la
biashara la kimataifa (metropolitan city), hapo ndipo tutakapoweza
kuifanya Dar es Salaam kama Dubai, Hongkong au Tokyo.
Dubai ni mji mkubwa, mzuri na maarufu, ndiko
kwenye majengo makubwa ya biashara, ndiko ambako uchumi wa nchi za Falme
za Kiarabu unakoonekana, lakini mji wa shughuli za Serikali ni
Abudhabi, mji tulivu na mwanana.
Kama mtu anataka kutafakari na kufanya kazi kwa
utulivu, Abudhabi ndiyo pahala pake, kama mtu anataka pilika na hamkani,
Dubai atakuwa amefika, hivyo si vibaya kuiga watu wa mataifa mengine
kwa mambo mazuri waliyofanikisha.
Nigeria nayo iliazimia kuhamisha mji wake mkuu,
kutoka Lagos kwenda Abuja mwaka 1976, dhamira hiyo ilikuja kufanikiwa
miaka 15 baadaye, lakini cha muhimu ni kuwa wameweza.
Hivyohivyo, Marekani, yenyewe iliondosha makao makuu ya Serikali
kutoka Washington DC na kuyapeleka New York, sababu za kufanya hivyo
ziko nyingi lakini la muhimu zaidi ni kupunguza msongamano wa mambo
katika eneo moja na kulipa eneo lingine nafasi ya kukua na kujitanua.
Ni kweli si rahisi kuhamisha shughuli za Serikali
kwa vuu, vuu, lakini miaka 38 si michache kwa mtu kujipanga na kutimiza
malengo, Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji Mkuu Dodoma, CDA, inapaswa sasa
ikamilishe mipango yote itakayoiwezesha Serikali kuhamia Dodoma. Hakuna
haja ya kusuasua tena, kwani ahadi za kuhamia Dodoma sasa zimekuwa ni
ahadi za kuku na vifaranga vyake, kila siku kesho na kesho haifiki.
Binafsi nadhani labda wakati Serikali inaweka
mikakati ya kuhamia Dodoma haikuweka muda, ilikuwa ni nadharia zaidi
kuliko vitendo.
Wakati umefika sasa wa kufupisha maneno na
kuongeza vitendo, ahadi ya serikali kuhamia Dodoma isiwe ahadi hewa.
Kipaumbele cha kwanza iwe ni kuhamisha Ofisi ya Rais na Ofisi ya Waziri
Mkuu, watu wawafuate viongozi hao Dodoma, hapo ndipo watakapoona ugumu
wa kuishi Dar es Salaam na kuwajibika Dodoma, kinyume cha hivyo tutakuwa
tunacheza makida makida tu.
Serikali kwa upana wake ikihamia Dodoma, tatizo la
foleni jijini Dar es Salaam litapungua. Hivi sasa mfanyakazi anatumia
zaidi ya saa tatu barabarani kabla hajafika kazini. Wakati wa kurudi
nyumbani tatizo huwa hilohilo, hivyo wengi huamua kutoka kazini kuanzia
saa mbili usiku ili kuepukana na foleni.
Hayo ni matatizo makubwa kiuchumi, kijamii na
kimaendeleo, watu hutoka nyumbani alfajiri na kurudi usiku, tafiti
zinaonyesha kuwa foleni ni sababu mojawapo ya ndoa nyingi kuvunjika.
Wazazi hawapati muda wa kukaa, kucheza na
kuzungumza na watoto wao, kila mmoja yuko katika mahangaiko ya maisha
huku foleni zikiongeza msongo wa mawazo.
Wana Dar es Salaam hawawezi tena kuhimizana muda,
kwani ‘zingatia kufika kwa wakati’ haina maana tena, hata mtu
akizingatia vipi, bado foleni itamkwaza, imekuwa vigumu kutimiza miadi
kwa wakati. Changamoto za foleni Dar es Salaam ni nyingi zisizoweza
kumalizwa na udadavuaji wangu leo, ila nisisitize tu kwamba wakati
umefika kwa Serikali kuhamia Dodoma.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment