Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Halmashauri zote nchini zimetakiwa
kutenga bajeti ya mwaka huu ya asilimia 60 ya makusanyo yake ya ndani
kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Bunge ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa bungeni jana kuhusu Utekelezaji wa Majukumu
ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Tamisemi,
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Hamis Kigwangala alisema kamati yake
haitakubaliana na bajeti ya halmashauri yoyote ile kama haijakidhi
matakwa ya agizo hilo na kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) imepewa
kazi kuhakikisha agizo hili la kamati linatekelezeka.
Dk Kigwangala alisema kamati inaendelea
kuzisisitiza sekretarieti za mikoa zikiongozwa na wakuu wa mikoa,
kuimarisha ufuatiliaji na kuzisimamia halmashauri na kuhakikisha kuwa,
fedha za miradi ya maendeleo zitokanazo na makusanyo ya ndani na nje
zinatumika kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema kamati yake pia imependekeza Serikali
kuweka mikakati madhubuti ya ukusanyaji wa mapato ya majengo katika
miji, manispaa, na miji midogo, kwani fedha nyingi zinapotea kwa
kutokusanywa kwa kodi hii.
Alisema kuwa Kamati inatambua kuwa agizo hili
limeshaanza kutekelezwa na Serikali, hata hivyo kwa yale maeneo ambayo
yameainishwa kutakiwa kufanyiwa tathimini kuhusu thamani halisi ya
majengo hayo kwa ajili ya kutozwa kodi ya majengo.
Alizitaka halmashauri kutumia mapato yake ya ndani
kukamilisha miradi ya ujenzi wa majengo ya madarasa, majengo ya
zahanati na vituo vya afya, nyumba za walimu, nyumba za wauguzi
vijijini, mabarabara ya vijijini, kuchimba visima.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment