Home » » 'MABALOZI WA NYUMBA 10 HAWAJUI KUSOMA'

'MABALOZI WA NYUMBA 10 HAWAJUI KUSOMA'

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
IMEELEZWA kuwa mabalozi wa nyumba 10 wanaochaguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hawajui kusoma wala kuandika hali inayorudisha nyuma maendeleo ya eneo husika.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, mjini Dodoma juzi Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilazo Kata ya Ipagala, Samwel Chimalusotola, alisema CCM inachagua wajumbe wa nyumba 10 kisiasa.
“Tatizo la CCM wanaangalia kadi ya chama na mavazi ya chama hicho hawaangalii upande wa elimu… nikiwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa natekeleza sera za CCM,” alisema Chimalusotola.
Alishauri mabalozi wachaguliwe na wananchi badala ya chama ili wawe chini ya wenyeviti wa serikali ya mtaa kwa lengo la kuleta maendeleo yenye tija.
 Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa