Home » » PINGAMIZI ZA ZITTO KABWE,CHADEMA KUSIILIZWA JULAI

PINGAMIZI ZA ZITTO KABWE,CHADEMA KUSIILIZWA JULAI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Zitto Kabwe
 
Pingamizi za awali za pande mbili katika shauri linalomhusu Mbunge wa Kaskazini, Zitto Kabwe na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yataanza kusikilizwa julai 31, mwaka huu.
Mashauri hayo yaliyopo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ni katika kesi iliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa.

Jaji John Utamwa, alisema kesi ilipangwa jana kwa ajili ya kutajwa na kwamba mapingamizi ya awali ya pande mbili yatasikilizwa siku hiyo.

Hata hivyo, wakati kesi hiyo ikitajwa jana, alikuwapo wakili Peter Kibatala wa Chadema lakini Zitto na wakili wake hawakuwapo mahakamani.

Katika kesi hiyo,  Zitto anaiomba mahakama kuiamuru Kamati Kuu na chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa katika Baraza Kuu la Chadema.

Aidha, mbali na kesi hiyo ya msingi, Jaji Utamwa alisikiliza maombi ya Zitto akiitaka itoe zuio la muda la kutojadiliwa uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Mahakama ilikubali katika uamuzi wake iliamuru Zitto asijadiliwe chochote kuhusu uanachama wake.

Aidha,  Zitto ameiomba mahakama imwamuru, Dk. Slaa kumkabidhi  nakala za taarifa na mwenendo mzima wa vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa katika ngazi ya juu ya chama hicho.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa