Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWENYEKITI wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage,
amewaonya wanachama kuwa makini kuelekea uchaguzi mkuu, kwani kitendo
cha kupandikiza maneno kwa Mgombea wa Urais Michael Wambura kitaharibu
mchakato mzima wa uchaguzi.
Uchaguzi Mkuu wa Simba unatarajia kufanyika Juni 29 mwaka huu, huku
leo ikiwa ni siku ya mwisho kuwasilisha pingamizi kuelekea usaili
unaotarajiwa kufanyika Mei 29 Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi mjini hapa, Rage alisema, wapo
wanachama wanasema Wambura sio mwanachama kitendo ambacho sio kweli,
huku akidai kuwa, katika kila jambo kuna taratibu za kufuata na kuwataka
wanachama kulitambua hilo.
Aidha, Rage alisema, mbali na hilo, pia endapo watafanya hivyo kutaka
kumuengua Wambura kwa kujtofuata taratibu, itawasababishia wao kupata
viongozi wabovu katika uchaguzi huo.
“Wapo wanaotaka Wambura afukuzwe uanachama, wengine wanasema sio
mwanachama, mpaka kufikia uamuzi huo kuna taratibu za kufuata ikiwemo ya
kumpa nafasi ya kusikilizwa, vinginevyo wataharibu uchaguzi au
watajikuta wanapata viongozi wabovu,” alisema Rage na kuongeza.
Nipo Dodoma, nafuatilia kwa karibu sana mchakato huu wa uchaguzi, wapo
wanaosema Wambura aenguliwe kwa sababu alienda mahamani, wengine
wanasema asigombee kwa sababu alishawahi kufukuzwa uanachama, mimi
nimeongoza vikao vyote vya Simba, sijawahi kuona Wambura anafukuzwa, au
anavuliwa uanachama, hiyo sio kweli kabisa,” alisema Rage.
Aliongeza kwa kuwaasa Simba kuwa makini na uchaguzi huo, kwani kama
wanataka kumuengua Wambura kuna taratibu za kufuata na lazima wampe haki
ya kusikilizwa.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment