Home » » SERIKALI ZA MITAA ZANYIMWA MABILIONI WANAWAKE,VIJANA

SERIKALI ZA MITAA ZANYIMWA MABILIONI WANAWAKE,VIJANA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Ludovick Utoh
Mamlaka za serikali za mitaa 68 kwa kushirikiana na serikali kuu hazikupeleka zaidi ya Sh. bilioni 10.9 za mfuko wa maendeleo ya wanawake na vijana kwa miaka mitatu, hivyo kukwamisha malengo ya mfuko ya kuwainua kimaendeleo.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imechanganua fedha hizo na kila halmashauri kuwa ni mwaka 2010/11 halmashauri 23 kila moja zaidi ya Sh. milioni 69, mwaka 2011/12 halmashauri 31 kila moja zaidi ya Sh.milioni 16.5 na mwaka 2012/13 halmashauri 68 kila moja Sh. milioni 160.

Alisema kwa mchanganuo huo, wastani wa fedha ambazo hazikupelekwa katika mfuko wa wanawake na vijana kwa halmashauri umeongezeka kwa zaidi ya Sh. milioni 143.9 (asilimia 87.2) ukilinganisha namwaka uliopita.

”Inaonyesha halmashauri hazikupeleka fedha kuchangia mfuko huo na hivyo kupelekea malengo ya uanzishwaji wake kutofanikiwa...Mamlaka za serikali za Mitaa ziweke mpango mkakati wa kupeleka fedha ambazo zilikuwa hazijapelekwa kwenye vikundi ili kuviwezesha kujiendesha na kumudu maisha na kutekeleza madhumuni ya kuanzishwa kwake,” alifafanua.

Aidha, ripoti hiyo imebainisha kuwa zaidi ya Sh. bilioni 1.4 zilizotolewa katika halmashauri 58 hazikurejeshwa ingawa muda wa marejesho ulikuwa tayari umeshapita hali inayoonyesha usimamizi usioridhisha katika ukusanyaji madeni, hivyo halmashauri kutokuwa na uwezo wa kuendelea kutoa mikopo zaidi kwa watu au vikundi vingine.
 
SOURCE: NIPASHE

Serikali za mitaa zawanyima mabilioni wanawake, vijana

13th May 2014
Print

0 comments:

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa