Home » » UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WATENGEWA SH.5 BILIONI

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WATENGEWA SH.5 BILIONI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwasilisha makadirio ya matumizi ya Ofisi yake na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2014/15, wakati wa kikao cha Bunge mjini Dodoma jana

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana aliwasilisha bungeni, bajeti ya ofisi yake na mfuko wa Bunge inayofikia Sh5.21 trilioni. Kati ya hizo, Sh5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Hayo yalielezwa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia wakati wa maelezo kuhusu kazi zilizotekelezwa mwaka 2013/2014 na mwelekeo wa kazi zitakazotekelezwa 2014/2015.
Ghasia alisema shughuli zitakazogharimiwa na fedha hizo ni pamoja na maandalizi ya masanduku ya kupigia kura, kupitia kanuni za uchaguzi na kuandaa fomu na nyaraka mbalimbali za uchaguzi.
Shughuli nyingine ni uhakiki wa majimbo ya uchaguzi huo ambayo ni vijiji, mitaa na vitongoji.
Malipo ya wabunge
Katika bajeti hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sh132.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya Mfuko wa Bunge la Muungano, kati yake posho na mishahara kwa ajili ya Bunge (wabunge na watumishi wa Bunge) ikiwa ni Sh123.94 bilioni.
Kwa mujibu wa nyaraka za bajeti hiyo, wabunge peke yao wametengewa Sh102.317 bilioni kwa ajili ya mishahara, posho za vikao na kujikimu na posho za safari ndani na nje ya nchi.
Kwa mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30 mwaka huu, mishahara na posho za wabunge zilitengwa Sh93.37 bilioni, kati ya hizo posho zilikuwa Sh48.74 bilioni ikilinganishwa na Sh49.526 bilioni zilizotengwa katika bajeti 2014/2015, sawa na ongezeko la Sh800 milioni.
Usimamizi wa rasilimali watu na utawala ambayo ndiyo inayohusika na mishahara na posho kwa watumishi wa Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015, umetengewa Sh21.6 bilioni.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa mishahara ya wabunge imetengewa Sh12.769 bilioni.
Safari za ndani
Posho za safari ndani ya nchi zimetengewa Sh11.192 bilioni wakati zile za safari za nje kwa wabunge zimetengewa Sh9.08 bilioni.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana aliwasilisha bungeni, bajeti ya ofisi yake na mfuko wa Bunge inayofikia Sh5.21 trilioni. Kati ya hizo, Sh5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Hayo yalielezwa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia wakati wa maelezo kuhusu kazi zilizotekelezwa mwaka 2013/2014 na mwelekeo wa kazi zitakazotekelezwa 2014/2015.
Ghasia alisema shughuli zitakazogharimiwa na fedha hizo ni pamoja na maandalizi ya masanduku ya kupigia kura, kupitia kanuni za uchaguzi na kuandaa fomu na nyaraka mbalimbali za uchaguzi.
Shughuli nyingine ni uhakiki wa majimbo ya uchaguzi huo ambayo ni vijiji, mitaa na vitongoji.
Malipo ya wabunge
Katika bajeti hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sh132.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya Mfuko wa Bunge la Muungano, kati yake posho na mishahara kwa ajili ya Bunge (wabunge na watumishi wa Bunge) ikiwa ni Sh123.94 bilioni.
Kwa mujibu wa nyaraka za bajeti hiyo, wabunge peke yao wametengewa Sh102.317 bilioni kwa ajili ya mishahara, posho za vikao na kujikimu na posho za safari ndani na nje ya nchi.
Kwa mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30 mwaka huu, mishahara na posho za wabunge zilitengwa Sh93.37 bilioni, kati ya hizo posho zilikuwa Sh48.74 bilioni ikilinganishwa na Sh49.526 bilioni zilizotengwa katika bajeti 2014/2015, sawa na ongezeko la Sh800 milioni.
Usimamizi wa rasilimali watu na utawala ambayo ndiyo inayohusika na mishahara na posho kwa watumishi wa Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015, umetengewa Sh21.6 bilioni.
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa mishahara ya wabunge imetengewa Sh12.769 bilioni.
Safari za ndani
Posho za safari ndani ya nchi zimetengewa Sh11.192 bilioni wakati zile za safari za nje kwa wabunge zimetengewa Sh9.08 bilioni.
Posho hizo ambazo hazikatwi kodi ni karibu mara nne ya kiwango kilichotengwa kwa ajili ya mishahara yao ambayo ndiyo pekee hukatwa kodi.
Fedha za Maendeleo
Kati ya Sh8.7 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo, Sh2.9 bilioni ni kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya Ofisi za Bunge, Sh5.9 bilioni ni kwa ajili ya programu ya kujenga miundombinu ya Bunge na programu ya kuimarisha Bunge imetengewa Sh755 milioni.
 Chanzo:Mwananchi

0 comments:

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa