Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Profesa Peter Msolla.
Aidha, Bunge halikuridhishwa na nyongeza kidogo ya Sh. bilioni 46.5 iliyotolewa kati ya jumla kuu iliyoidhinishwa na Bunge jambo lililoifanya wizara hiyo nyeti kuwa na upungufu wa Sh. bilioni 127. 2 na kushindwa kukamilisha miradi mingi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Profesa Peter Msolla, alisema pengo hilo limesababisha wizara hiyo kukwama kutekeleza karibu miradi yote kwa vile kati ya miradi 1,473 iliyokuwa itekelezwe iliyokamilika ni 228 .
“Bila fedha hizi kutolewa hakuna muujiza utakaoiwezesha wizara kufikia malengo ya kuwafikishia wananchi maji hasa wa vijijini ambako tatizo ni kubwa zaidi.”
Profesa Msolla alisema Bunge linaitaka serikali kutoa fedha hizo kama zilivyoidhinishwa ili Wizara itekeleze malengo iliyokusudia.
Mwaka huu wa fedha serikali ilikuwa imeipangia wizara hiyo bajeti ya Sh. bilioni 138 kwa ajili ya miradi ya maji, lakini Bunge liliongeza Sh. bilioni 184.4 na kuifanya ifikie Sh. bilioni 312.1.
Pia, kamati aliihoji serikali kuhusu kutokamilika kwa miradi mikubwa ya maji ambayo imechukua muda mrefu kama ile ya Kimbiji , Mpera pamoja ujenzi wa bwawa la Kidunda, upanuzi wa vyanzo vya maji vya Ruvu Juu na Chini.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment