Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Serikali imeendeleza kigugumizi cha kutoruhusu mikutano ya hadhara katika mikoa ya Lindi na Mtwara hadi hapo itakapotangazwa.
Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuwa akijibu swali la Seleman Bungala (Lindi Vijijini-CUF).
Mbunge huyo alitaka kauli ya Serikali kuhusu
kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na taasisi za kidini katika mikoa ya
Lindi na Mtwara kama bado zuio hilo lipo na ni sababu zipi zilisababisha
kutolewa kwa amri hiyo.
Bungara (Bwege) alisema hivi sasa kumekuwa na
utulivu wa kutosha katika mikoa hiyo jambo linasababisha wananchi kuhoji
juu ya viongozi hao kutofanya mikutano.
Waziri Mkuu alikiri Serikali kuzuia mikutano
katika mikoa hiyo kutokana na ukaribu wake na hasa yaliyotokea Mtwara
wakati wa vurugu za gesi.
Alisema bado anafuatilia kupitia vyombo mbalimbali
na kuona hali haijatulia bado, lakini ukifika wakati akijiridhisha,
ataruhusu mikutano hiyo kuendelea.
“Unajua hivi karibuni nilitaka kuruhusu mikutano
ya Lindi iendelee kufanyika lakini kuna mambo fulani hayaja kaa sawa,”
alisema Pinda.
Alisema ataendelea kufuatilia kupitia vyombo
mbalimbali pamoja na wakuu wa mikoa hiyo na akijiridhisha ataruhusu kwa
kuwa hata yeye na chama chake wanahitaji kuzungumza na wananchi kwa kuwa
uchaguzi mkuu wa mwakani hauko mbali.
Wakati huohuo, Pinda ametangaza kuwa hakuna
mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) atakayeshindwa kufanya
mitihani yake ya mwisho kwa sababu ya kukosa ada.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment