Home » » 'SERIKALI KUKOPA BENKI ZA NDANI KUMEONGEZA RIBA'

'SERIKALI KUKOPA BENKI ZA NDANI KUMEONGEZA RIBA'

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Esther Matiko
Riba katika benki na asasi za fedha imeendelea kuwa juu kutokana na serikali kuwa mmoja wa wakopaji wakubwa kutoka katika mabenki na asasi za fedha hapa nchini.
Akiwasilishwa Bungeni taarifa ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu mpango wa maendeleo wa taifa mwaka 2014/15, Esther Matiko, alisema, Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania iliyotolewa Machi 2014 imeanisha kuwa serikali imekopa kutoka kwenye vyanzo vya ndani zaidi ya Sh. trilioni moja katika kipindi cha Machi 2013 hadi Machi 2014.

Alisema hali hii imesababisha ushindani usio wa  haki baina ya serikali na wananchi wanaokopa katika mabenki hayo na anayeumia kwa hii ya ushindani ni mkopaji mdogo.

Alisema ukopaji wa serikali unachangia kufanya riba ziwe juu. Riba inayolipwa na serikali kwa “Treasury Bills” ya mwaka mmoja mpaka mwezi Desemba 2013 ilikuwa asilimia 15.63.

Alisema pamoja na kuwepo na mabenki mengi mfumo wa fedha haufanyi kazi ya kukusanya akiba kwa wingi na kuiwekeza kwa wajasiriamali wa ndani ili kukuza uchumi na kuongeza ajira.

Matiko alisema kupungua kwa riba za beki kutaongeza fursa za kukopa na kusaidia wananchi kukuza mitaji na hali hii itasaidia ongezeko la ajira ambalo ni tatizo kubwa nchini.

Akisoma maoni hayo kwa niaba ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Matiko aliongeza kuwa kukua kwa uchumi wa taifa, idadi ya walipa kodi itaongezeka na ustawi wa wananchi utaimarika.
 
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa