Home » » TAZAMA PICHA 10 ZA AJALI KIBAIGWA ,MH MWIGULU AJITOA KUSAIDIA MAJERUHI‏

TAZAMA PICHA 10 ZA AJALI KIBAIGWA ,MH MWIGULU AJITOA KUSAIDIA MAJERUHI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Gari Ndogo ya Toyota Rav 4 ikiwa imepinduka eneo la Kibaigwa


Mashuhuda wa ajali hiyo wakitoa msaada wa kulinyanua akiwemo Mh Mwigulu Nchemba


 Mh:Mwigulu Nchemba akisaidia kuoka Majeruhi kwa Kuinua gari.
 Gari aina ya RAV4 ikiwa imeshainuliwa tayari na Majeruhi wametoka walikuwa wawili.


Kazi ya Kuondoa Betri ya Gari ndio inafanyika ilikuepusha Moto
 Huyu ndiye alikuwa Dereva wa gari hii iliyopata ajali,amepata Michubuko kidogo
Ajali ndogo Imetokea maeneo ya Kibaigwa ikihusisha gari aina ya RAV4 iliyokuwa ikitokea Mkoani Morogoro kwenda Dodoma,Ajali hiyo mbayo haijasababisha Kifo chochote imetokea majira ya Mchana na Sababu ya ajali inatajwa kuwa ni Mwendo kasi wa Dereva na hatimaye Gari Kumshinda na kupinduka.

Katika hali ya Kuonesha Ubinadamu na Utu kwa Watu Wengine,Mh:Mwigulu Nchemba aliyekuwa akitoka Dodoma kuelekea Morogoro kwenye Mkutano alilazimika Kusimama kwa Muda kwenye ajali hiyo kwaajili ya Kutoka Huduma ya Kwanza kwa Majeruhi kama anavyoonekana Pichani hapo Juu.Jambo hilo liliwafurahisha sana Wananchi waliokuwa eneo la ajali na waliomba Viongozi wengine waige tabia hii ya Mwigulu Nchemba ya Kushirikiana na Wananchi wakati wa Shida husuasani wanapoona ajali barabarani,Ugonjwa,Misiba n.k wajitahidi kutoa Ushirikiano.
Picha/Maelezo na Sanga Jr.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa