Home » » UZINDUZI WA WA KAMPEINI YA KUTOKOMEZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO WAFANYIKA DODOMA CHINI YA MRADI WA SHIRIKA LISILO LA LA KISERIKALI LA TUNAJALI‏

UZINDUZI WA WA KAMPEINI YA KUTOKOMEZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO WAFANYIKA DODOMA CHINI YA MRADI WA SHIRIKA LISILO LA LA KISERIKALI LA TUNAJALI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Bilson Vedastus - Dodoma
Hatimaye serikali ya mkoa wa Dodoma imewaongoza wakazi wa mkoa wa Dodoma katika uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto chini ya mradi wa shirika lisilo la kiserikali la TUNAJALI sambamba na uwasilishaji wa dawa ya kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi ya OPTION B. 

Akizungumza wakati wa zoezi la uzinduzi wa kampeni hiyo iliyobeba kauli mbiu ya Pima mapema anza tiba yakiwa na lengo la kupunguza maambukizi hadi kufikia asilimia sifuri ifikapo mwaka 2025 uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jana juni 18 mwaka huu,afisa tawala mkoa wa Dodoma Rehema Madenge alisema kuwa ni wajibu wa jamii kupambana na maambukizi kwa kupima afya zao kwa hiari.

Aidha katika hatua nyingine Bi Madenge aliongeza kuwa serikali ya mkoa wa Dodoma imejipanga katika kuhakikisha wanadhibiti maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI ambapo amedai kuwa bado wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika wilaya zote za mkoa wa Dodoma.

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika uzinduzi huo wamelipongeza shirika la TUNAJALI kwa kuendesha zoezi la kupima Afya bure ambapo wameiomba serikali kuunga mkoano mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kuomba maadhimisho hayo yawe endelevu.

Naye meneja uhusiano wa shirika hilo Bi Agnes Kabigi amesema kuwa mpango huo unalenga kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto chini ya asilimia sifuri kufikia mwaka 2025 ambapo amewashukuru wakazi wa Dodoma kwa kujitokeza kuunga mkono kampeni hiyo.


DODOMA YETU 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa