Home » » WAFANYAKAZI WATISHIA KUANDAMANA BUNGE LA KATIBA

WAFANYAKAZI WATISHIA KUANDAMANA BUNGE LA KATIBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Jaji Joseph Warioba.
 
Wafanyakazi wametishia kuandamana hadi katika jengo la Bunge la Katiba mjini Dodoma, endapo wajumbe wa Bunge hilo watakaporejea wataendelea kujadili hoja nje ya rasimu iliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wfanyakazi (Tucta), Hezron Kaaya, wakati akifunga mafunzo ya viongozi wa vikundi vya wafanyakazi kutoka maeneo mbalimbali ya vyama vya wafanyakazi nchini.

Alisema wafanyakazi wamechoshwa kuona wabunge wakijadili masuala yao binafsi huku wakiweka kando rasimu ya katiba yenye maoni ya wananchi na wafanyakazi.

“Nasema hivi hawa wabunge wakiendelea na kujadili hoja zao binafsi nje ya rasimu iliyotumia fedha nyingi kwenye tume kutafuta maoni yetu, tutaandamana hadi mjengoni (bungeni) na kuwaondoa wabunge hao,” alisema.

Hezron alidai kuwa, kilichokuwa  kikiendelea ndani ya Bunge la Katiba kabla ya kuahirishwa ni masuala ya watu binafsi, huku ya wananchi yakiwekwa pembeni, jambo ambalo alisema halikubaliki.

Alisema kitu kikubwa anachoshangaa na kuwashangaza wafanyakazi wengi ni pale wanaposikia kuwa baadhi ya wajumbe wana mpango wa kubadilisha baadhi ya vifungu kuhusu suala la watumishi wa umma kwa kuwapunguzia madaraka.

Alisema maoni hayo hayajatolewa na tume bali yalitolewa na wafanyakazi kwa lengo la kuweka misingi imara ya utawala bora.
 
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa