Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JUMLA ya sh. bilioni 491 zinatumika kujenga barabara ambazo zinazunguka mji wa Dodoma kutokana na mkoa huo kukua kwa kasi.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli hivi karibuni alipokuwa akizindua taa za barabarani mjini Dodoma.
Dk. Magufuli alisema kuwa serikali imewekeza mabilioni ya fedha
katika mji wa Dodoma, kwa ajili ya ujenzi wa barabara zinazounganisha
mji huo.
“Kwa sababu ukitoka Dodoma kwenda Iringa barabara ya lami inajengwa
na inakaribia kumalizika, kutoka Dodoma mjini hadi Mayamaya, Bonga hadi
Babati kuna makandarasi wanajenga na kutoka hapa kwenda Central Cordor
zimeishamalizika, na kutoka hapa hadi Dar es Salaam zimeishamalizika.
“Pamoja na barabara za mjini kumalizika, tunaendelea kujenga barabara
nyingine za kutoka Dodoma mjini kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma, na miradi
hii yote kwa ujumla wake ina zaidi ya sh bilioni 491,” alieleza.
Mbali na hilo, Dk. Magufuli alisema kuwa Dodoma ni makao makuu ya
nchi, hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha inajengwa kwa kiwango
ambacho kitakubalika
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment