Home » » MOTO MKUBWA WAZUKA NA KUTEKETEZA MADUKA KATIKA SOKO LA MITUMBA JAMATINI MKOANI DODOMA

MOTO MKUBWA WAZUKA NA KUTEKETEZA MADUKA KATIKA SOKO LA MITUMBA JAMATINI MKOANI DODOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Baadhi ya watu wa mji wa Dodoma wakisaidia kuzima moto uliokuwaukiendelea kuteketeza mabanda ya wafanyabiashara katika soko la mitumba la jamatini maarufu kama Sarafina baada ya moto huo kuzuka kuanzia kwenye banda la vinyago usiku wa kuamkia leo.
  Wafanyabiashara katika eneo la Sarafina manispaa ya Dodoma wakisikitika walipokuwa wakiangalia moto uliokuwa ukiteketeza mabanda pamoja na mali zilizokuwa ndani, chanzo cha moto huo bada hakijajulikana.
 Wakazi wa Dodoma Wakijaribu kuudhibiti moto mkubwa uliokuwa ukiteketeza mali na mabanda ya wafanyabiashara wa mitumba katika eneo la jamatini  kwa kutumia mchanga na matawi ya miti ili usiendelee baada ya kudumu zaidi ya saa tatu huku zaidi ya mabanda 80 yakiteketea
 Moto mkubwa ukiendelea kuteketeza mabanda ya wafanyabiashara wa maduka na mitumba katika eneo la Sarafina Dodoma
 Bidhaa mbalimbali zikiwa zimezagaa baada ya kutolewa kwenye moja ya mabanda yaliyokuwa yakiungua kutokana na moto ambao bado haujajulikana chanzo chake katika eneo la nyuma ya kituo cha Daladala jamatini Dodoma.
Wafanyakazi wa Zimamoto wakiendelea kuwajibika wakati walipokuwa wakizima moto katika eneo la jamatini linalopakana na baa ya Actik, ambapo zaidi ya vibanda 80 viliteketea zikiwemo mali za wafanyabiashara wa eneo hilo lililopo manispaa ya Dodoma
PICHA NA JOHNBANDA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa