Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, amesema
pamoja na uchumi kuonekana umekua, bado uwiano kati ya wenye nacho na
wasiokuwa nacho ni mkubwa.
Mukoba alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya uzinduzi wa baraza kuu
la tatu la wafanyakazi katika utumishi wa umma Tanzania Bara
lililofanyika mjini hapa.
Alisema inashangaza kuona kipindi ambacho inasemekana kuwa uchumi wa
nchi umekua ndicho kipindi ambacho watumishi wamekuwa wakifanya vibaya
zaidi, jambo ambalo linatia shaka na kuonyesha wazi kuwa watumishi bado
wana madai ambayo hayatekelezeki.
“Miaka ya 1980 watumishi walikuwa wakitembea mwendo mrefu kufuata
mishahara ama kufuata mahitaji kutokana na miundombinu mibovu, lakini
miundombinu mizuri, lakini watumishi wanafanya kazi vibaya tofauti na
miaka hiyo, hapo inaonyesha kuwa ni kutokana na kutokuwepo kwa mgawanyo
wa rasilimali za nchi zilizopo. Lipo kundi dogo ambalo linapata
mgawanyo mkubwa wa rasilimali na kundi kubwa linapata rasilimali kidogo
za nchi,” alisema.
Awali Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Pindi
Chana, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, alisema hivi sasa
wananchi wanazielewa haki zao na wanaweza kudai huduma bora na kuhoji
utendaji wa serikali kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment