Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) inakusudia kuanza
mchakato wa kuifanyia marekebisho sheria yake Septemba mwaka huu, ili
kuiwezesha kutoza faini watu watakaopatikana na bidhaa bandia ama
zisizokidhi viwango.
Hayo yalisemwa jana na meneja wa Kanda ya Kati wa TFDA, Florent Kyombo, alipokuwa akizungumzia tatizo la vyakula na dawa bandia.
Alisema sheria ya sasa inairuhusu mahakama kutoza
faini badala ya mamlaka, jambo ambalo limekuwa likifanya utoaji adhabu
kuchukua muda mrefu. “Septemba mwaka huu mamlaka itaanza kupitia upya
ili tutoze faini sisi badala ya kwenda kortini,” alisema. (Sharon Sauwa)
Chanzo:Mwnanchi
Chanzo:Mwnanchi
0 comments:
Post a Comment