Home » » TEMBO,FARU HATARINI KUTOWEKA

TEMBO,FARU HATARINI KUTOWEKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Tembo, faru hatarini kutowekaVITENDO vya ujangili vinavyoendelea kushamiri nchini, vimechangia taifa kukumbwa na hatari ya kutoweka kwa wanyamapori wakiwemo tembo na faru.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa na Profesa Davis Mwamfupe wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  alipokuwa akitoa mada kwenye semina ya kuwajengea uelewa wabunge katika kulinda wanyamapori, iliyoandaliwa na Chama cha Wabunge cha Kuhifadhi na Kulinda Wanyamapori.
Profesa Mwamfupe alisema hivi sasa wanyama hao ambao walikuwa wengi katika mbuga na hifadhi mbalimbali nchini, wamepungua kwa kiasi kikubwa.
Alisema hakuna takwimu zinazoonyesha kuongezeka kwa wanyama hao, bali kupungua kutokana na vitendo vya ujangili.
Alieleza kuwa hali hiyo inatokana na uelewa mdogo wa wananchi kuhusiana na faida za wanyamapori.
“Hali hii ndiyo iliyotupa mwamko wa kutoa elimu kuhusiana na hifadhi za wanyamapori na thamani ya wanyama hao, lakini pia hali halisi inayoendelea hivi sasa kuhusiana na wanyamapori,” alisema.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa