Home » » WATUMISHI SERIKALI ZA MITAA WALALAMIKIWA

WATUMISHI SERIKALI ZA MITAA WALALAMIKIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SERIKALI imekiri kuwa watumishi wa Serikali za Mitaa wanalalamikiwa na wananchi kwa kufanya kazi zao kinyume cha maadili.
Taarifa ya malalamiko hayo ilitolewa mjini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celine Kombani.
Taarifa hiyo ilisomwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Fatuma Ally kwa niaba ya Waziri Kombani.
“Katika ziara hizo nimepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na watumishi wa umma juu ya vitendo ambavyo ni kinyume na misingi ya utawala bora.
“…Malalamiko mengi yanasababishwa na kutowajibika vema kwa watendaji wa shughuli za serikali, hasa kwenye mamlaka za serikali za mitaa.
“Malalamiko mengi ni matumizi mabaya ya madaraka, kushuka kwa maadili, rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za umma,” alisema Fatuma kwa niaba ya waziri huyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wapo baadhi ya makatibu tawala wa wilaya wanaofanya kazi kwa mazoea na hawaendani na mabadiliko ya mfumo.
“Pale ambapo baadhi yao watashindwa kuwajibika au kutozingatia misingi ya utawala bora hatua zitachukuliwa dhidi yao,” alisema mkuu huyo wa wilaya.
Chanzo;Tanzania Daima  

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa