Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WIZARA ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi imetakiwa kuhakikisha
inawapa washindi wote zawadi walizoahidi katika kilele cha maonyesho ya
Nanenane 2013 kabla ya kuanza kwa maonyesho ya Kanda ya Kati Agosti
mosi mwaka huu ili kuondoa ubabaishaji.
Agizo hilo limetolewa mjini hapa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.
Rehema Nchimbi, wakati wa kikao cha pili cha maandalizi ya maonyesho na
mashindano maalumu ya mifugo kitaifa na maonyesho ya Nanenane Kanda ya
Kati.
Alisema kitakuwa kitendo cha aibu kama wataanza mashindano mengine bila kuwakabidhi zawadi zao washindi wa mwaka jana.
Kwa upande wake, wizara hiyo ilisema juhudi zinaendelea ili
kutekeleza ahadi hiyo kabla ya kuanza kwa maonyesho ya mwaka huu, licha
ya kuwa Dk. Nchimbi aliyakataa majibu hayo na kutaka waeleze kwa uwazi
zaidi.
Baada ya Dk. Nchimbi kupingana na majibu hayo, walieleza kuwa
wanachosubiri ni fedha za matumizi ya kawaida ya ofisi (OC), ya Julai
mwaka huu ambayo bado hazijatoka na mara tu zitakapotoka, watawapa
washindi wote zawadi zao.
Katika hatua nyingine, Tanzania Daima ilifanya mahojiano na
baadhi ya washindi kwa sharti la kutotajwa majina yao kuhusu jambo
hilo, ambao wametishia kuandamana kuhakikisha wanapewa zawadi zao kabla
ya washindi wa mwaka huu.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment