Home » » JK: BADO NINA MAMLAKA KUTIMUA MA-RC, MA-DC

JK: BADO NINA MAMLAKA KUTIMUA MA-RC, MA-DC

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

>RAIS Jakaya Kikwete amesema bado anayo mamlaka ya kuwafuta kazi wateule wake wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya ambao watashindwa kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za kata ifikapo Novemba mwaka huu.
Pia amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali kusimamia maendeleo ya wanafunzi ili kuondoa kabisa tatizo sugu la wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaokwama masomo yao njiani waweze kubainika na kurejeshwa shuleni.
Mbali na hilo ameagiza kuchukukiwa hatua kali kwa watu wanataobainika wamewaozesha wanafunzi wao wa kike na waoaji wakamatwe na kufunguliwa mashitaka ya sheria ya ubakaji kwa vile mwanafunzi hapaswi kuolewa kabla ya kumaliza masomo yake.
Rais alirejea kutoka kauli hiyo wakati wa hotuba yake ya majumuisho yaliyofanyika juzi katika ukumbi wa Sekondari ya Gairo ikiwa ni kuhitimisha ziara yake ya wiki moja mkoani Morogoro aliyoianza Agosti 20 mwaka huu na kuzitembelea wilaya zote sita za mkoa huo.
“Tumeambizana kuhusu ujenzi wa vyumba vya maabara tatu, kasi yake ni ndogo , sitaki kusema sana hapa ...msidhani nimesahau nasubiri muda tuliowekeana ukifika, kwa vile bado nina mamlaka na viongozi niliowateua, wale watakaoshindwa kukamilisha maabara sitakuwa na huruma nao,“ alisema Rais.
Kuhusu wanafunzi kukatisha masomo yao, Rais akionesha kusikitishwa na hali hiyo hasa kwa Wilaya ya Mvomero , Kilombero na Kilosa.
Alitumia fursa hiyo kuwaagiza viongozi wa wilaya na Mkoa wa Morogoro kukaa na kujadili namna ya kukabiliana na tatizo la sugu la wanafunzi wanaoshindwa kumaliza elimu ya msingi na kidato cha nne.
Chanzo;Habari Leo 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa