Home » » WAANDISHI WADAI KUWA MAKONDA ANAWASUMBUA

WAANDISHI WADAI KUWA MAKONDA ANAWASUMBUA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Paul Makonda juzi alishitakiwa kwa Mkurugenzi wa Habari za Bunge, Jossey Mwakasyuka kwamba amekuwa akiwasumbua waandishi wa habari wanaoripoti habari za bunge hilo.
Malalamiko hayo yalitolewa na mmoja wa waandishi wa habari katika kikao baina yao na uongozi unaoshughulikia habari bungeni hapo.
Makonda alitajwa kikaoni hapo kwamba amekuwa akiwafuata waandishi wa habari na kuwasumbua pale anapoona habari zilizoandikwa hazina mwelekeo wa habari ambazo anazitaka yeye.
“Mkurugenzi, naomba utusaidie . Kama mjumbe Paul Makonda ni msemaji wetu wanahabari au ndiye aliyetumwa kutukosoa, inasikitisha kuona anatusumbua,” alisema mmoja wa waandishi wa habari anayeandikia gazeti moja la Kiingereza.
Mkurugenzi huyo alipokea taarifa hiyo na kuahidi kuifanyia kazi kwa kuwasiliana na Makonda.
Hata hivyo, katika kuonyesha umuhimu wa jambo hilo, dakika chache baada ya kikao kumalizika, Makonda alipita na kuelekea ofisini kwa mkurugenzi huyo ambako haikujulikana walizungumza nini, lakini iliwachukua zaidi ya dakika 30.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa