Home » » WAJASILIAMALI 100 WAKUTANA

WAJASILIAMALI 100 WAKUTANA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
MAONESHO ya wafanyabiashara kipindi cha Bunge la Maalum la Katiba yanaendelea kwa kasi mjini hapa na kuwakutanisha wajasiriamali zaidi ya 100 katika viwanja vya Mashujaa.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa wajasiriamali, Dokta Haruna Kifimbo, alisema lengo kuu la maonesho hayo ni kutoa fursa kwao kuuza na kunadi bidhaa zao kwa watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Bunge hilo.
“Mpaka sasa tuna wajasiriamali 100,  ambao wanaendelea na maonesho  yao kwenye viwanja hivi vya Mashujaa kuanzia Agosti 10 mwaka huu, na maonesho yataendelea mpaka litakapomalizika Bunge la Katiba, hivyo bado tunaendelea kupokea wajasiliamari wengine zaidi,” alisema Dk. Kifimbo.
Alisema kuwa maonesho hayo yanajumuisha wauzaji wa bidhaa za tiba mbadala, bidhaa za majumbani, kazi za mikono kutoka ndani na bidhaa zingine mbalimbali.
Kifimbo ambaye ni mganga wa tiba mbadala alisema maonesho hayo yatazinduliwa rasmi Agosti 21, mwaka huu, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, na kutoa rai kwa wananchi kushiriki.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa