Home » » DK. KEBWE AZINDUA ‘TUIMARISHE AFYA’

DK. KEBWE AZINDUA ‘TUIMARISHE AFYA’

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen KebweNAIBU Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Stephen, amezindua mradi ujulikanao kama ‘Tuimarishe Afya’ mkoani hapa, akisema Tanzania inashika nafasi ya pili barani Afrika katika usambazaji dawa na vifaa tiba.
Mradi huo, ambao Dk. Kabwe amesema ni wa kwanza kufanyika nchini, utaziwezesha wilaya saba za Mkoa wa Dodoma kuagiza dawa kwa kutumia mfumo wa utaratibu wa kupitia kwa muuzaji mkuu, ili kuweza kukidhi mahitaji ya dawa zinazosambazwa na Bohari Kuu ya Madawa (MSD).
Alisema kuwa mikoa mingine itapaswa kuja Dodoma kwa ajili ya kujifunza juu ya maradi huo, ambao utasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto ili wakautekeleze.
Dk. Kebwe, aliisifu MSD kwa kazi nzuri waliyoifanya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994, licha ya kuwepo changamoto kubwa ya matakwa ya wadau kwamba wawe na mshindani.
Kwa mujibu wa Prof. M. Meshack, kiongozi wa timu ya mradi wa Health Promotion and System Strengthening (HPSS), mradi huo ni sehemu ya ushirikiano baina ya Uswisi na Tanzania katika kuleta maendeleo.
Alisema kuwa, mradi huo ulizinduliwa mwaka 2011 ukiwa umelenga kuusaidia Mkoa wa Dodoma kwa miaka 10 katika sekta ya bima ya afya, uboreshaji wa afya ya jamii, usimamiaji wa dawa na usimamiaji wa matengenezo ya vifaa vya afya.
“Mradi huu wa HPSS umefadhiliwa na ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na unatekelezwa na shirika la Ujerumani la The Micro Insurance Academy (MIA), pamoja na shirika la The Ifakara Health Institute la Tanzania.
Prof. Meshack aliongeza kuwa, ili kuboresha upatikanaji wa dawa, wilaya saba za Dodoma pamoja na viongozi wa mkoa na kwa msaada wa mradi wa HPSS wameamua kutumia mbinu ushirikiano na sekta binafsi yaani Public-Private-Partnership (PPP), ambapo Bahari Ltd ndiye muuzaji mkuu aliyechaguliwa.
Chanzo; Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa