Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WABUNGE
wanawake nchini, wameazimia kuunda kamati ndogo ya wataalamu
itakayowashirikisha wanawake kutoka katika mabunge ya Kenya, Rwanda na
Uganda ili kutafuta mfumo sahihi wa uwakilishi wa uwiano wa asilimia 50
kwa 50.
Azimio hilo limefikiwa juzi mjini hapa, katika semina ya siku mbili
ya mradi wa kuwajengea uwezo wabunge (LSP), iliyoandaliwa na Bunge la
Jamhuri ya Muungano chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP).
Wazo la kufikia uamuzi huo, lilitolewa na mwanaharakati wa masuala ya
jinsia, Prof. Ruth Meena, wakati akichangia mada iliyotolewa na Rais wa
Wabunge Wanawake Bunge la Afrika, Bernadeta Mushashu, iliyohusu namna
ya kuongeza wanawake kufikia 50:50.
Prof. Meena, alisema kuwa pamoja na suala la usawa wa jinsia
kukubaliwa na pande zote za wanawake na wanaume, anaona bado kuna hofu
na hivyo kupendekeza iundwe kamati hiyo ili upatikane mfumo sahihi ambao
utajulikana mapema uweze kuzoeleka.
Katika mada yake, Mushashu alielezea aina tofauti ya mifumo hiyo ya
uwakilishi, faida na changamoto zake, kisha akawataka wanawake wachague
mfumo uliyo sahihi.
Alisema mfumo wa kwanza ni kuwa na wabunge wawili wawili kila jimbo,
ambako watapigiwa kura na wananchi katika jimbo zima la uchaguzi. Kwamba
ukichukulia majimbo ya sasa yalivyo, jumla ya wabunge itakuwa 2
x239=478.
Mfumo wa pili ni wa halmashauri kutambuliwa kuwa jimbo, ambapo
kutakuwa na wabunge wawili kila jimbo (halmashauri). Kwa mfumo huo jumla
ya wabunge itakuwa halmashauri Tanzania Bara + Zanzibar = 168 +10
(2×178= 356).
“Mfumo wa tatu ni kuendelea kuwa na wabunge wa majimbo. Pia kuwe na
wabunge wanawake kwenye ngazi ya Wilaya. Wanawake wa vyama vyote
wagombee hiyo nafasi ya kiti cha Wilaya na wapigiwe kura na wakazi wote
katika wilaya husika. Hii itafanya jumla ya wabunge wote kufikia, (jimbo
+ wilaya Bara + Zanzibar) 239 + 133 + 10 = 382,” alisema Mushashu.
Aliongeza kuwa, pia kuwe na kiti cha mbunge mwanamke kwenye ngazi ya
halmashauri ili wanawake wa vyama vyote wagombee hiyo nafasi ya kiti cha
halmashauri na wapigiwe kura na wakazi wote katika halmashauri hiyo.
Kwamba hiyo itafanya jumla ya wabunge wote kufikia (jimbo +
halmashauri)= 239 + 168 + 10 = 417.
halmashauri)= 239 + 168 + 10 = 417.
Naye mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah aliwatahadharisha wanawake
kwamba mfumo huo wa uwiano wa jinsia unaopendekezwa wa asilimia 50/50
hautatumika katika uchaguzi mkuu ujao 2015, ikiwa hawatasimamia suala
hilo liingizwe kwenye mabadiliko ya 15 ya katiba ya mwaka 1977
yatakayofanyika
Chanzo:Tanzani Daima
0 comments:
Post a Comment