Home » » JAMII YAASWA MAPAMBANO DHIDI YA MIHADARATI

JAMII YAASWA MAPAMBANO DHIDI YA MIHADARATI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, ametoa wito kwa jamii kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kuwa vita hiyo ni ya kimataifa.
Misime, alitoa wito huo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kukabidhiwa cheti cha pongezi kwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya dawa ya kulevya mkoani Dodoma, kilichotolewa na mtandao wa Saada, ambao unajishughulisha na mapambano dhidi ya mihadarati mkoani hapa.
Kamanda Misime, alisema kuwa madhara ya dawa za kulevya hayana mwenyewe, hivyo ni jukumu la familia na jamii kwa ujumla kuwa mstari wa mbele katika kukomesha vita hivyo, kwa kuwa madhara yake ni makubwa hasa kwa vijana.
Alitoa wito kwa familia, kuwaelimisha vijana wao kuhusiana na madhara ya dawa za kulevya, kwa kuwa familia zina nguvu kubwa kuliko hata jeshi la polisi katika kukemea matumizi ya dawa hizo.
“Familia bado zina jukumu kubwa la kutoa elimu kwa vijana wao kuhusiana na matumizi ya madawa ya kulevya, kwa kuwa huathiri akili za vijana na nguvu kazi ya Taifa, hivyo kama familia itachukua hatua katika vita hii ni dhahiri kuwa mapambano yake yatakuwa rahisi,” alisema Misime.
Kwa upande wake, Mratibu wa shirika la Saada, Ismail Kaitilla, alisema vijana ambao wanatolewa kwenye matumizi ya dawa za kulevya, wanatakiwa uangalizi wa karibu ili wasiweze kurejea katika matumizi hayo.
Alisema jukumu hilo ni la familia zenye vijana ambao wameachana na matumizi ya dawa za kulevya, ili vijana hao wasirejee tena katika matumizi hayo hatari.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa