Home » » SUNGURA ALAANI MTOTO KUBAKWA, KUUAWA

SUNGURA ALAANI MTOTO KUBAKWA, KUUAWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

NAIBU Waziri kivuli wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sabrina Sungula, amelaani kitendo cha mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi jijini Dar es Salaam kuuwawa kikatili baada ya kubakwa, kuchinjwa na kunyofolewa sehemu zake za siri
Akizungumaza na Tanzania Daima  jana, Sungura ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), alisema kitendo hicho kinalitia doa taifa na kuonyesha kuwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji vinaendelea kwa kasi kubwa.
Alieleza akiwa Waziri kivuli mwenye dhamana, anaitaka serikali kuhakikisha inakomesha vitendo vya aina hiyo, ili hata wale ambao wanafikiria kuendeleza unyama huo waache mara moja.
Sungura alitoa kauli hiyo siku chache  baada ya kuripotiwa kutokea ukatili huo kwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka saba.
Katika tukio hilo, mama wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa), alisema baada ya mwanawe kurejea toka shuleni alimuogesha na kumpa chakula cha jioni, alitoka kidogo na aliporejea nyumbani  hakumkuta na ndipo alipokwenda kwa majirani kumtafuta.
Alisema mpaka saa moja usiku hakufanikiwa kumuona mtoto huyo licha ya kuambiwa mara ya mwisho alionekani akiwa anacheza na mtoto wa jirani yake.


Hata hivyo, siku ya tukio majira ya saa 2 asubuhi, alipata taarifa ya kuonekana kwa mwili wa mtoto wake kwenye shamba moja  lililopo karibu na nyumbani kwake.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa