Home » » WANANCHI WADAI KUCHOSHWA NA LUSINDE

WANANCHI WADAI KUCHOSHWA NA LUSINDE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Livingstone Lusinde
WANANCHI wa Mtera wameeleza kuchoshwa na mbunge wao Livingstone Lusinde (CCM), kwa madai kuwa ni mzigo kutokana na kutumia muda mwingi kutukana wapinzani badala ya kujenga hoja za maendeleo.
Wakizungumza katika mkutano wa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutoka kanda ya Magharibi, Kati na wa Mkoa wa Dodoma, wananchi hao walielezwa kuchoshwa na michango ambayo haina taarifa ya mapato na matumizi.
Mmoja wa wananchi hao, Elia James, alisema licha ya Serikali kudai elimu ya Msingi ni bure, wanafunzi wameendelea kufukuzwa kwa kudaiwa michango huku wazazi wakiwekwa mahabusu na kutozwa faini ya sh 45,000.
Christopher Peter, alisema kituo cha afya cha Handali hakina dawa, hivyo wananchi wanalazimika kwenda umbali mrefu kutafuta dawa, jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa kero kubwa ya afya huku mbunge wao akitumia muda mwingi majukwaani na bungeni kutukana wapinzani badala ya kuwa na hoja ya kuwasaidia wananchi wake.
Alisema kuwa mbunge huyo amekuwa ni mtu wa kutukana akiwa majukwaani na kuwadanganya wananchi kuwa atawaletea maendeleo, bila kuwaambia ukweli kuhusu fedha za mfuko wa jimbo jinsi zinavyotumika kwa ajili ya maendeleo.
Akiwahutubia wananchi hao, Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Magharibi, Christopher Nyamwanji, alisema CCM ni mzimu ambao hautaki wananchi wapate maendeleo, na kuwataka kuhakikisha hawafanyi makosa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 5 mwaka huu
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa