Home » » WAISLAMU WASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE ELIMU

WAISLAMU WASHAURIWA KUWEKEZA KWENYE ELIMU

WAUMINI wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuwekeza mali na fedha zao kwenye elimu hususan kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na yatima ili waweze kujikwamua kimasomo.
Ushauri huo umetolewa na Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Kata ya Chang’ombe, Bashiru Hassein, alipokuwa akizungumza na waumini wa dini hiyo kwenye sherehe za mwaka wa kiislamu iliyofanyika uwanja wa shule ya Chang’ombe Dodoma mjini.
Hussein, alitumia muda huo kutoa taarifa mbalimbali za kiutendaji zinazofanywa na baraza hilo, ikiwemo ya kuwahudumia kimasomo yatima 600.
Katibu huyo, alisema wakiwezeshwa kielimu kuna uwezekano mkubwa wa kuwaondolea pia umaskini na hata ile dhana potofu iliyojengeka ya kutegemea kufadhiliwa na kuomba omba ya kila mara wataondokana nayo.
Katika sherehe hiyo, Bakwata Kata ya Chang’ombe, ilipokea msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo vya kompyuta, mashine ya ‘photo copy’ na vipaza sauti vyenye thamani ya sh milioni 1.9, ambavyo vilitolewa na Mkurugenzi wa Islamic Centre Dodoma, Taji  Mohamed.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa