Home » » DKT. TULIA AKSON AWA NAIBU SPIKA MPYA WA BUNGE‏

DKT. TULIA AKSON AWA NAIBU SPIKA MPYA WA BUNGE‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Lilian Lundo
Maelezo
Dodoma
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Mhe.Dkt. Tulia Akson kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka Chama cha Wananchi (CUF) Mhe. Magdalena Sakaya.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mhe. Dkt. Akson  kushinda kwa kura 250 ambazo ni sawa na asilimia 71.2 za kula halali dhidi ya mpinzani wake Mhe. Sakaya aliyepata kura 101 ambazo ni sawa na asilimia 28.8 ya kura halali.

Uchaguzi huo umefanyika leo, Mjini Dodoma ambao ulitanguliwa na uthibitisho wa jina la Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Akiomba kura kwa wabunge Mhe. Dkt. Akson alisema kuwa atajitahidi   kuwatunukia wananchi wote bila kujali tofauti za kisiasa ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Aliongeza kuwa atajitadi kumshauri  vizuri Spika juu ya Sheria na Kanuni kwa kutumia  uzoefu alionao  kama Mwanasheria mzoefu ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.

Akimpongeza  Mhe. Dkt. Akson Tulia kwa ushindi alioupata, Mhe. Sakaya  alisema kuwa matarajio yake na  watanzania ni kuona nchi inakuwa na Bunge imara litakalo fanya kazi zake kwa uimara bila ubaguzi ili kuiletea nchi maendeleo.

Akitoa neno la shukurani mara baadaya kuchaguliwa  Mhe. Dkt. Akson  alimshukuru Mhe. Rais kwa uteuzi alioufanya wa kumteua kuwa Mbunge na hatimaye kugombea nafasi ya Naibu Spika wa Bunge la 11.

“Naahidi nitawatumikia kama mtumishi wenu, tutafanya kazi kiufanisi  na pia nitatumia weledi wangu katika kazi zangu kama Naibu Spika, naomba msisite kuniletea hoja zenu pale mnapokuwa nazo,” alisema  Mhe. Dkt . Akson.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika Mhe. Dkt. Akson alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali .
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa