Home » » Chenge awafunda wabunge kuhusu kanuni za Bunge

Chenge awafunda wabunge kuhusu kanuni za Bunge

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Mwenyekiti wa kikao cha Bunge ambaye pia Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge amewataka wabunge kujifunza kwa umakini namna bora ya kutumia kanini za Bunge.

Mwenyekiti Chengeamefanya hivyo mara kadhaa alipokuwa akijibu miongozo ya wabunge kutoka vyama vya upinzani wakiwamo Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (CHADEMA), Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT) pamoja na Mbunge wa Singida Magharibi Tundu Lissu (CHADEMA).

Kwa upande wa Kubenea ameomba muongozo kuhusu mbwa walioingizwa Bungeni na askari polisi wanaume kuwapekua wanawake jambo ambalo ahaliruhusiwi kwa kanuni ambapo Mwenyekiti wa Bunge amemtaka mbunge huyo kutafuta kanuni nyingine ya kupeleka ombi lake kama anadhani hoja yake ni ya msingi.

Kwa upande wa Lissu pamoja na Zitto wenyewe wameomba miongozo kuhusu mpango wa serikali wa miaka mitano uliowasilishwa na serikali kupitia wizara ya fedha,kwamba umekiuka kanuni za bunge,ambapo mwenyekiti akawajibu kwamba mpango haujakiuka na sii mara ya kwanza kufanya hivyo.

Aidha Mwenyekiti wa Bunge ametoa rai kwa wabunge wote kuzisoma kanuni za bunge na kuzielewa na mipaka yake katika namna bora ya kuendesha vikao hivyo vya Bunge.

Hata hivyo Kikao cha bunge kimeendelea na shughuli zake huku wabunge wa kambi rasmi ya upinzani wakirejea baada ya kugomea kushiriki katika mjadala wa kuijadili hotuba ya Rais kwa kigezo cha shirika la utangazaji la Taifa kutorusha matangazo ya moja kwa moja kuhusiana na mijadala hiyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa