Home » » Serikali imepokea taarifa za kuzama kwa kivuko

Serikali imepokea taarifa za kuzama kwa kivuko

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Serikali imesema imepokea kwa masikitiko taarifa za kuzama kwa Kivuko cha mto kilombero na kewamba kamati za ulinzi na usalama zipo katika eneo hilo kuhakikisha hali inarejea salama katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa Bungeni na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu) Jenista Mhagama baada ya kutakiwa afanye hivyo na naibu spika wa Bunge Tulia Mwansasu kuhusiana na suala hilo.

Mheshimiwa Naibu spika serikali imepata taarifa hizo kwamba kivuko hicho kilikuwa kimebeba watu 31 na magari na mizigo mbalimbali na kilizama jana usiku ambapo watu 30 wameokolewa huku jitihada mbalimbali zikiendelea kuleta usalama katika eneo hilo.

Aidha Waziri Mhagama amewataka wananchi kuwa makini kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa nchi itapata mvua nyingi sana pamoja na upepo mkali hivyo ni vyema wasafiri wakawa makini katika maeneo mbalimbali.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa