Home » » UHABA WA FEDHA WAKWAMISHA MIRADI.

UHABA WA FEDHA WAKWAMISHA MIRADI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani.
Serikali imesema kukosekana kwa fedha za kutosha kumechangia baadhi ya miradi ya maendeleo kusimama ikiwano ya barabara.
 
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, aliyetaka kujua ni lini serikali itapeleka fedha kwa mkandarasi  ili aweze kumaliza ujenzi wa daraja la Kilombero.
 
Ngonyani alisema fedha za ujenzi wa daraja hilo zinatolewa na serikali kwa asilimia 100 lakini haiwezi kukamilisha miradi yote kwa wakati mmoja kutokana na uwezo wa mdogo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani.
 
Alisema ujenzi wa daraja hilo unatarajia kukamilika Desemba mwakahuu.
 
Akijibu swali la msingi lililohoji ni lini seriklai itaanza kumaliza ujenzi wa barabara ya Kidatu, Ifakara na Mlimba kwa kiwango cha lami.
 
Alisema barabara ya Kidatu hadi Ifakara mradi huo umeanza kutekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha na katika awamu ya kwanza na ya pili jumla ya kilomita 16.17 zilijengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa