Home » » Wabunge upinzani wanyimwa mwongozo,wasusia bunge

Wabunge upinzani wanyimwa mwongozo,wasusia bunge

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wabunge wa Upinzani wameendelea na mgomo wao wa kutoka nje ya ukumbi wa bunge baada ya kikao cha bunge kumaliza muda wa maswali na majibu kwa serikali.

Hali hiyo imetokea baada ya Naibu Spika Tulia Mwansasu amemtaka katibu wa bunge kuarifu bunge ratiba inayoendelea, ambapo katibu wa bunge alibainisha kwamba kazi ya ratiba ya leo inaonyesha kwamba ni kuchangia hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa bunge.

Baada ya hapo wabunge wa upinzani waliomba miongozo kutoka kwa Naibu spika ambapo Naibu spika amemruhusu Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko ambapo Mbunge huyo ameuliza swali kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa elimu bure kwa wanafunzi kutozwa michango katika jimbo lake.

Naibu wa spika akitoa majibu ya muongozo huo ambapo amesema kwamba serikali inatanbua matatizo yanayojitokeza na inayafanyia kazi

Jambo hilo limewakasirisha wabunge wa upinzani na kuzidi kuomba miongozo ambapo Naibu Spika amewakataza na kuruhusu ratiba iliyo mbele ya bunge kuendelea,hali ambayo imewafanya wabunge wa upinzani kutoka nje.

Hata hivyo wabunge wa upinzani baada ya kutoka nje hapo jana walishinikiza kwamba hawawezi kukubali serikali kuendesha mikutano ya Bunge bila kuonyesha live kwa kisingizio cha fedha kukosekana.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa