Home » » KAMATI YA BUNGE YATAKA MASHIRIKA YA UMMA YASIMAMIWE KWA UKARIBU.

KAMATI YA BUNGE YATAKA MASHIRIKA YA UMMA YASIMAMIWE KWA UKARIBU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwenyekiti wa PIC, Richard Ndassa.
Kamati  ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji (PIC) imeishauri serikali kusimamia mashirika ya umma ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha ambazo serikali imewekeza katika mashirika hayo.
 
Akizungumza baada ya kikao cha mafunzo ya kamati hiyo na Msajili wa Hazina jana, Mwenyekiti wa PIC, Richard Ndassa, alisema, kamati yake ina majukumu ya kusimamia mashirika ya umma ambayo yako zaidi ya 260, mengi yakionekena kuwa na kasoro ikiwamo matumizi makubwa kuliko mapato.
 
“Tumekuwa tukishuhudia mashirika mengi ya umma yanatumia fedha nyingi katika kushughulika na masuala yasiyo na msingi kulinganisha na mapato wanayokusanya licha ya kuwa serikali inawekeza fedha nyingi kuendesha mashirika haya,” alisema  Ndassa.
 
 Awali, Msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru, aliiomba kamati hiyo kushirikiana na serikali katika kushauri namna bora ya uwekezaji katika mashirika ya umma.
 
Alisema kwa kufanya hivyo, kutawezesha faida inyopatikana kuendana na uwekezaji pamoja na kuwa na sheria madhubuti itakayoainisha usimamizi bora wa mashirika na kuondoa mgongano wa majukumu katika usimamizi wake.
 
Akiwasilisha mada kuhusu majukumu na muundo kwa ofisi  ya Msajili wa Hazina mbele ya Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Serikali, alisema serikali imekuwa ikiwekeza pesa nyingi lakini faida inayopatikan ni ndogo.
 
Alisema kiwango cha matumizi katika mashirika hayo ya umma kimekuwa kikubwa kulinganisha na mapato ya ndani. Alisema  kumekuwapo na ongezeko la matumizi kutoka asilimia 83 mwaka  2011/2012 hadi asilimia 86 mwaka 2014/15.
 
Kuhusu deni la taifa, Mafuru alisema limekuwa likiongezeka kutokana mashirika ya umma kukopa katika kuendeleza miundombinu lakini yamekuwa yanashindwa kurudisha na kuiachia mzigo serikali.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa