Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanza
kufanya tathmini ya utendaji wa mabaraza ya watoto ngazi za kata,
wilaya, mkoa na taifa katika mikoa sita ya Tanzania bara.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk
Hamis Kingwangala alisema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la
Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema) Katika swali lake, Mnyika
alitaka kufahamu lini serikali itawasilisha taarifa ya tathimini ya
utendaji wa mabaraza ya watoto na walemavu na serikali imefikia hatua
gani katika kuwezesha kufanya kazi kwa baraza la vijana la taifa baada
ya sheria yake kupitishwa.
Dk Kingwangala alisema tathmini imeanza kufanyika katika mikoa sita
nchini, lengo kuu lake ni kubaini hatua zilizofikiwa katika utekelezaji
wa malengo ya mabaraza kama ilivyokusudiwa katika uanzishwaji wake.
Alisema hilo litakamilika Mei mwaka huu na mara baada ya kukamilika
Wizara itaandaa ripoti ambayo itaonesha matokeo ya tathmini ya utendaji
wa mabaraza katika ngazi zote na kuiwasilisha kwa wadau.
Alisema baraza la taifa la ushauuri la watu wenye ulemavu
lilizinduliwa Novemba mosi, 2014 lakini kutokana na ufinyu wa bajeti
baraza hilo lilifanya kikao chake cha kwanza Januari 14 na 15, 2016.
Alisema serikali itafanya tathimni na kutoa taarifa baada ya
kumalizika kipindi cha mwaka mmoja baada ya baraza hilo kuanza kufanya
kazi.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment