Home » » MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (Kulia) pamoja na Waziri wa Elimu,Ufundi,Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Joyce Ndalichako wakiwasili katika ukumbi wa Bunge kushiriki kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
 Askari wa Bunge akiweka Siwa katika ukumbi wa Bunge kuashiria kuanza kwa kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
  Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson akiongoza kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
 Naibu wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji wakatiakitoa Taarifa ya Utendaji wa  Soko la Bima Nchini kwa kipindi cha Mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba,2014 wakati wa  kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
 Waziri wa Elimu,Ufundi,Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Joyce Ndalichako akiwasilisha Taarifa ya mwaka ya chuo Kikuu Cha Dodoma kwa mwaka wa Fedha 2013/2014 katika kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi wakati wa katika kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.

Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa