Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini Joseph Msukuma Kasheku (CCM)
ameiomba serikali kufanya utafiti wa kina kati ya madawa ya kulevya ya
mirungi,bhangi na pombe za makaratasi maarufu kama viroba nini kina
madhara zaidi kwa vijana.
Mbunge huyo ameyasema hayo katika kikao cha 5 cha bunge la 11 linaoendelea na vikao vyake katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma.
''Mheshimiwa mwenyekiti zao la mirungi na bhangi kuna nchi zinaruhusu
mfano majirani zetu wa Kenya ndege mbili kubwa hutua nchini humo
kuchukua mirungi na kupeleka ulaya sasa kwa nini sisi tusiendeleze zao
hili linalopatikana Geita na maeneoya Bunda mkoani Mara na maeneo
mengine nchini ili wananchi wanufaike kwa kuuza zao hilo lakini nchi
ipate fedha za kigeni pia''
Msukuma ameongeza kuwa ''kwa wasukuma kule kwetu mtu akitumia bhangi
analima sana hata hekari mbili lakini inakatazwa na wakati huo huo
vijana hawa wanadhoofika kwa viroba hivyo tufanye utafiti ili kama
viroba ndivyo vyenye athari zaidi vipigwe marufuku.
Wakati huo huo Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika Dkt Khamis Kigwangalla
amesema madawa ya kulevya ya bhangi na mirungi yana athari kubwa sana za
kiafya na hasa afya ya ubongo na serikali kwa namna yoyote haitakubali
kuruhusu au kujadili kwa namna yoyote kuhalalishwa kwa madawa hayo.
0 comments:
Post a Comment