Home » » MBUNGE ATUHUMU KITENGO CHA INTELEJENSIA WANYAMAPORI.

MBUNGE ATUHUMU KITENGO CHA INTELEJENSIA WANYAMAPORI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imeshauriwa kuchunguza kwa kina wafanyakazi wa Idara ya Wanyamapori Kitengo cha Intelijensia kutokana na kile kilichoelezwa bungeni kwamba wanashirikiana na majangili.
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora (CCM) alitoa angalizo kwa Serikali jana bungeni wakati akichangia mwongozo wa mapendekezo ya mpango wa taifa wa maendeleo wa mwaka mmoja.
Alisema ili kuinua Pato la Taifa ni lazima serikali ishughulike na ujangili unaotishia kwenye mapori pamoja na watalii wanaoingia nchini akisema wapo baadhi ya polisi waliofukuzwa, lakini wameajiriwa ndani ya idara hiyo jambo alilosisitiza kuwa ni hatari.
“Naomba nikujulishe Mheshimiwa Maghembe (Profesa Maghembe- Waziri wa Maliasili na Utalii), hii mambo ya kuandika humu kwamba tunataka kuboresha miundombinu, kununua zana za kupambana na majangili...maana yake tukiendelea kukupa zana za kupambana na majangili, wanaendelea kuzitungua (akimaanisha helikopta),” alisema.
Aliendelea kusema, “Na kwenye idara yako ya wanyamapori, na kwenye hifadhi yako ya Ngorongoro ndiko kuna wafanyakazi wasio waaminifu, kwenye Idara ya Intelijensia ambao wanaazimisha silaha za kivita, wanawapa majangili halafu wanatungua ndege.”
Kwa mujibu wa Lugora, mmoja wa watuhumiwa wa kuangusha ndege iliyosababisha kifo cha rubani hivi karibuni, aliajiriwa na idara hiyo licha ya kuwa amefukuzwa kwa uhalifu. Alisisitiza kuwa bila wafanyakazi wa idara husika kuchunguzwa na kusimamiwa, nchi itaendelea kuwa na majangili hata kama serikali italeta zana za kisasa.
Akizungumzia mpango wa Serikali wa kutaka taasisi zake pamoja na halmashauri kuweka fedha za makusanyo kwenye mfuko wa pamoja wa Hazina, mbunge huyo alisema mapendekezo hayo ni mazuri.
CHANZO : HABARI LEO.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa