Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imeongeza juhudi kuhakikisha wanaojihusisha na biashara
haramu ya dawa za kulevya wanakamatwa na kuadhibiwa vikali kupitia
Sheria Namba 5 ya Mwaka 2015.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na
Ajira, Dk Abdallah Possi alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mwantumu Dau Haji (CCM). Katika swali
lake, mbunge huyo alitaka kufahamu serikali imejipanga vipi kuona
inawanusuru vijana katika janga la dawa za kulevya.
Akijibu swali hilo, Dk Possi alisema serikali inatambua kuwa matumizi
ya dawa za kulevya yana madhara mengi kwa watumiaji, familia na jamii
kwa ujumla. Dk Possi alisema ili kunusuru vijana na madhara hayo, hatua
mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuendeleza huduma njema na
endelevu ya serikali ya kutoa matibabu kwa watumiaji wa dawa za kulevya
katika hospitali na vituo vya magonjwa ya akili ili kuwasaidia watumiaji
wa dawa hizo.
Alisema hatua nyingine zilizochukuliwa ni kuratibu na kusaidia
kuanzishwa kwa nyumba za ushauri na upataji nafuu na huduma za kuwafikia
watumiaji katika miji mbalimbali nchini. Dk Possi alisema hatua
nyingine ni kuanzisha huduma ya tiba kwa kutumia dawa ya methadone
kwenye hospitali. Akijibu swali la nyongeza la mbunge huyo, Dk Possi
alisema mtu yeyote mwenye taarifa ya askari wanaowalinda watumiaji wa
dawa za kulevya waziwasilishe.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment