Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
achague
SERIKALI imesema itaendelea kufanya mabadiliko katika sheria ili kupunguza misamaha ya kodi.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema
hayo bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo
Peneza (Chadema) ambaye alitaka kujua serikali inachukua hatua gani ili
kuondokana na misamaha ya kodi inayotolewa kwa kampuni za uwekezaji.
Alisema serikali inaendelea kufanya mabadiliko katika sheria hiyo ili
kupunguza misamaha ya kodi inayotolewa kwa ridhaa, yaani misamaha
inayotolewa kwa kampuni moja moja kwa mikataba na kwa kupitia katika
mamlaka ya waziri wa fedha na mipango.
Alisema ili kuboresha kivutio cha msamaha kwa wawekezaji kodi imekuwa
ikipunguzwa katika bidhaa na shughuli za jumla. Pia misamaha ya kodi ni
moja ya vivutio vinavyotolewa kama moja ya njia ya kuwahamasisha
wawekezaji ili waTanzania badala ya kwenda nchi nyingine.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment