Home » » WAFICHUENI ASKARI WANAOWALINDA WAUZA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

WAFICHUENI ASKARI WANAOWALINDA WAUZA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dk. Abdallah Possi.
Wananchi wametakiwa kutoa taarifa dhidi ya askari ambao wanadaiwa kuwafumbia macho wanaojihusisha na biashara za dawa ya kulevya ili wachukuliwe hatua.
 
Wito huo ulitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dk. Abdallah Possi, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantumu Haji, aliyehoji ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya askari ambao wanafumbia macho wauza dawa za kulevya.
 
Haji alisema kuna askari ambao hawaendani na kasi ya kuthibiti dawa za kulevya na kuhoji ni mbinu gani zinazotumika kuthibiti tatizo hilo.
 
Dk. Possi alisema askari kutochukua hatua  shidi ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ni kinyume cha sheria na kufanya hivyo ni kosa la jinai.
 
“Kwa wale ambao wanawafahamu askari wanaojihusisha na suala hili watoe taarifa ili wachukuliwe hatua,” alisema.
 
Aidha, akijibu swali la msingi la mbunge huyo, aliyehoji serikali imejipanga vipi kunusuru vijana katika janga  la utumiaji wa dawa za kulevya, Dk. Posi alisema serikali inatambua maumizi ya dawa za kulevya yana madhara mengi kwa watumiaji, familia na jamii kwa jumla, hivyo imejipanga kupambana na tatizo hilo.
 
Alisema ili kuwanusuru vijana serikali imechukua hatua kwa kuongeza juhudi za kimkakati za kuhakikisha wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wanakamatwa na kuadhibiwa vikali.
 
Alisema serikali pia inaendelea kutoa matibabu kwa watumiaji wa dawa za kulevya katika hospitali na vituo vya magonjwa ya akili nchini ili kuwasaidia watumiaji wa dawa hizo kuacha.
 
CHANZO: NIPASHE.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dodoma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa